Mabosi Gor kutua rungu kali

Muktasari:

Kumekuwa na hali ya sintogahamu ndani ya klabu hiyo kwa wiki kadhaa sasa, masaibu ambayo yamechangia wao kubanduliwa nje ya dimba la CAF Confederation Cup na RS Berkane wa Morocco waliowalima magoli 2-0 Nairobi na kishwa kuwabomoa mengine 5-1 kwenye mechi ya marudiano kule kwao Casablanca.

HUKO Kogalo bado moto unawaka. Safari hii Mwenyekti wa Gor Mahia, Ambrose Rachier amesema klabu hiyo itawachukulia hatua kali wachezaji Francis Kahata na Philemon Otieno miongoni mwa wengine kwa kuiharibia jina uongozi na kuchora taswira mbaya kuwa klabu inawanyanyasa.

Kumekuwa na hali ya sintogahamu ndani ya klabu hiyo kwa wiki kadhaa sasa, masaibu ambayo yamechangia wao kubanduliwa nje ya dimba la CAF Confederation Cup na RS Berkane wa Morocco waliowalima magoli 2-0 Nairobi na kishwa kuwabomoa mengine 5-1 kwenye mechi ya marudiano kule kwao Casablanca.

Kasheshe ndani ya klabu zilianza kwenye mechi ya kwanza iliyochezewa nyumbani ambapo wachezaji wa Gor waligoma kushiriki mazoezi siku mbili kabla ya pambano lenyewe, wakilalamikia kutolipwa bonsai zao za mechi walizoshinda tangu mwaka jana.

Lakini kwenye kikao na wahabari Rachier, Rachier aliwapasha kinoma wachezaji hao, akitaka wafahamu kuwa hakuna sheria inayoishurutisha klabu kuwalipa bonasi hizo wanazodai kwa sababu huo huwa ni uamuzi wa kibinafsi wa klabu yeyote duniani kuwatuza wachezaji wenzake.

“Nataka niweke hili wazi kwamba wachezaji wote walilipwa mishahara yao ya Mwezi Machi pesa taslimu siku mbili kabla ya mchuano wa kwanza dhidi ya RS Berkane. Walitakiwa kuingia kambini kama ilivyoada ila waliamua kususa ili kulalamikia bonasi. Labda tu waelewe hili, hamna sheria yeyote katika ulimwengu wa soka unaotambua bonasi kama hizi. Utoaji wa bonasi hizo huwa ni mapenzi na uamuzi wa klabu yeyote ile duniani ila sio kwamba ni lazima” Rachier akawapasha.

Vile vile alikana madai kuwa uongozi ulisafiri kuelekea Casablanca kwa kutumia tkiketi za First Class huku wachezaji wakisafiri kwa Economy Class ambapo baadhi yao waliishia kutaabika safarini kiasi cha kuwalazimun kulala katika uwanja wa ndege.

Picha za Kahata na Otieno ndizo zilizosambaa mitandaoni zikiwaonyesha wawili hao wakiwa wamelala kwenye sakafu za uwanjani wa ndege kule mjini Doha.

“Kikosi kizima cha Gor na benchi la ukufunzi pamoja viongozi sote tulisafiri kwenye mazingira sawa ambayo yalikuwa magumu kwetu sote.

Kulikuwa na matatizo ya usafiri wa ndege na ndio sababu sote tulichelewa kufika kwa wakati ukizingatia tiketi tulipewa na serikali kwa kuchelewa.

Zile picha zilizosambaa za wachezaji wawili wakiwa wamelala sakafuni zililenga kuchora taswira ya wanavyoteseka, lengo likiwa ni kuiharibia jina na sifa uongozi. Hili halitapita hivyo, lazima tutalifranyia kazi.

Tunaendelea kuchunguza na nawahakikishieni wote waliohusika watachukulia hatuan kali za kinidhamu” Rachier aliwaka zaidi.

Aidha kiongozi huyo alihoji ni kwa nini kama kweli wachezaji hao walikuwa wakiteseka, mbona hawakuposti picha walipobukiwa kwenye hoteli ya kifahari ya Laico mjini Nairobi pake ndege walilopaswa kusafiri nalo lilipopata matatizo.