Mabadiliko ya ratiba yawatesa Simba, Yanga

Muktasari:

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera juzi alilalamikia kitendo cha bodi ya ligi kubadilisha ratiba pasipo kuzingatia afya za wachezaji.

Dar es Salaam.Bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TBL) imebadilisha mara tatu muda wa kucheza mechi kati ya Simba na Kagera Sugar.
Jana bodi ya ligi ilipanga mechi ya Simba na Kagere ipigwe saa 10:00 badae wakabadilisha ichezwe saa 8:00 kisha wakarudisha saa 1:00.
Hiyo sio mara ya kwanza kwa bodi hiyo kwani hata mechi zilizopita kati ya Yanga na Mtibwa Sugar, Simba na Coastal Union walirudisha muda nyuma badala ya kucheza saa 10:00 ikapigwa saa 8:00.
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera juzi alilalamikia kitendo cha bodi ya ligi kubadilisha ratiba pasipo kuzingatia afya za wachezaji.
"Mechi inapigwa saa nane, halafu wanakuwa wanabadilisha gafra hiki sio kitu kizuri kwani kinakuwa kinaumiza wachezaji na kutuchanganya makocha"alisema.