Lyon yaitanguliza Simba, nane walioiua Yanga waanzia benchi

Muktasari:

Kocha wa Simba amewaanzisha wachezaji watatu waliocheza mechi iliyopita waliopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga.

Arusha. Simba imekuwa ya kwanza kuingia uwanjani saa 8:40 mchana mapema kabla ya wenyeji wao African Lyon kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Simba inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara imeingia uwanjani hapo na kupokewa na mashabiki wake, huku African Lyon ikiingia uwanjani saa 8:50 mchana.

Kikosi cha Simba leo kitawakosa washambuliaji wake nyota wa kimataifa, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi beki Juuko Murshid kwa sababu mbalimbali.

Kocha Partick Aussems amefanya mabadiliko ya wachezaji nane walioanza dhidi ya Yanga leo wapo benchi.

Wachezaji pekee waliocheza dhidi ya Yanga walionza leo ni kipa Aish Manula, beki Pascal Wawa na nahodha John Bocco.

Kikosi cha Simba: Kipa Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante kwasi, Bukaba Bukaba, Pascal Wawa, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Adam Salamba, John Bocco na Rashid Juma.

Kikosi cha African Lyon: Douglas Kisembo, Halfani Mbaruku, Omary Salum, Ronand Msonjo, Emmanuel Simwanza, Jabir Azizi, Pato Ngonyani, Awadh Juma, Stephano Mwasyika, Said Mtikila na Ramadhani Chombo.