Lupita azidi kutikisa tuzo za Oscars

Tuesday February 26 2019

 

By Thomas Matiko

Nairobi. MWIGIZAJI Lupita nyong’o kwa mara nyingine tena alifunika kwenye tuzo za hadhi za Oscars zilizofanyika mapema Jumatatu.

Japo hakushinda tuzo la kibinfasi, filamu aliyoigiza mwaka jana akiwa mojawepo wa wahusika wakuu ‘Black Panther’ ilishinda tuzo tatu.

Lupita hakuficha furaha yake akitoa taarifa akisema “Nashukuru kuwa mojawepo wa wadau katika safari hii. Acha nisubirie kuona mengi yakayofuata. Wakanda forever”

Filamu hiyo iliyozua gumzo kote duniani na pia kuingiza kipato kikubwa cha mamilioni ya dola sokoni, iliibuka bingwa kwenye vitengo vya tuzo za Best Costume Design, Best Production Designe na Best Original Score.

Kwenye Makala hayo ya 91, waandalizi walijitahidi kuepukana na skendo za ubaguzi wa kirangi ambazo zimekuwa zikizonga makala ya awali kwa kuhakikisha kuwa tabaka  tofauti tofauti ya jamii iliibuka na tuzo.

Kwa mfano tuzo zilizotwaliwa na ‘Black Panther’ ambayo waigizaji wake kwa asilimi 90% walikuwa wenye asili ya watu weusi.

Vile vile mwelekezi mkongwe Spike Lee ambaye kwa miaka mingi ameishi kukosoa tuzo hizo akizitaja kuwa za kibaguzi zilizolenga kuwatuza wazungu, aliibuka na tuzo la Best Adapted Screeplay kupitia filamu yake ya ‘BlackkKlansman’

Advertisement