Luhende awapa neno wenzake

Muktasari:

Luhende amesema soka ni kazi yao hivyo kusimama kwa dharula hakuwapi nafasi wao kuona wapo huru na kuanza kushusha kiwango.

 BEKI wa Kagera Sugar, David Luhende amesema kipindi hiki kinahitaji wachezaji kujitambua zaidi kuhakikisha wanalinda viwango vyao.
Luhende amesema soka ni kazi yao hivyo kusimama kwa dharula hakuwapi nafasi wao kuona wapo huru na kuanza kushusha kiwango.
Amesema bila kusukumwa kila mchezaji analazimika kupambana ili ligi ikianza awe kwenye ushindani.
"Hakuna kulala, tukizidisha mazoezi, naamini pamoja na changamoto ya corona tutakuwa na ushindani mkubwa," anasema
"Katika maisha ili ufanikiwe inahitaji kujituma kwa bidii hapo utajitofautisha na wengine"amesema.
Amesema ligi ikiendelea itapima uwezo wa wachezaji jinsi walivyojitunza viwango vyao nje na usimamizi wa makocha.