Luhende: Kila mtu ajitambue

Muktasari:

"Unajua kuna kufanya mazoezi ili watu wakuone, pia yapo yale ya kumsaidia mchezaji kumfanya kuwa fiti na pumzi ya kutosha hao wote ni rahisi kuonekana ndani ya dakika 90,"amesema.

BEKI wa Kagera Sugar, David Luhende amesema anatambua majukumu yake jambo linaloondoa hofu ya kucheza chini ya kiwango ligi ikianza.

Luhende amesema kazi yao inawataka muda wote miili yao iwe  tayari kwa ajili ya majukumu akimaanisha kufanya mazoezi kuwa sehemu ya maisha yao.

"Ukizungumzia mchezaji kujitambua ni jinsi anavyokuwa yupo kwenye kiwango cha juu muda wote hii ina maana kwamba anakuwa rafiki wa mazoezi,"

"Unajua kuna kufanya mazoezi ili watu wakuone, pia yapo yale ya kumsaidia mchezaji kumfanya kuwa fiti na pumzi ya kutosha hao wote ni rahisi kuonekana ndani ya dakika 90,"amesema.

Amesema asipofanya mazoezi basi mwili wake anakuwa anahisi amepungukiwa hivyo inakuwa inamlazimu kila siku awe anajifua.