Liverpool inazungumza na staa wa Ivory Coast

Muktasari:

Lille inataka dau la Pauni 70 milioni kwa staa huyo ambaye pia amekuwa akiandamwa zaidi na Bayern Munich lakini inafahamika Liverpool kwa sasa inaongoza katika mbio za kumng’oa Ufaransa.

RAIS wa Lille ya Ufaransa, Gerard Lopez amethibitisha Klabu ya Liverpool inafanya mazungumzo na staa wao wa kimataifa wa Ivory Coast, Nicolas Pepe lakini klabu hiyo ya Anfield bado haijaanza kufanya mazunguzo rasmi na wao kuhusu staa huyo.

Pepe ambaye kwa sasa yupo na Ivory Coast katika michuano ya Mataifa ya Afrika kule Misri amekuwa akiwaniwa na klabu kubwa za Ulaya baada ya kutesa msimu uliopita akiwa na Lille akifunga zaidi ya mabao 20 ya msimu.

Lille inataka dau la Pauni 70 milioni kwa staa huyo ambaye pia amekuwa akiandamwa zaidi na Bayern Munich lakini inafahamika Liverpool kwa sasa inaongoza katika mbio za kumng’oa Ufaransa.

Winga huyo wa kimataifa wa Ivory Coast akitumia sana mguu wa kushoto kama staa mwingine wa Liverpool, Mohamed Salah na tetesi zinadai anaweza kuwa mrithi wa kudumu wa nyota huyo wa Misri pale Anfield.