Liverpool baba lao zimebaki pointi 12 kutwaa ubingwa wa Epl

Muktasari:

Ikiwa  Liverpool wataendelea kucheza kwenye kiwango chao, basi wanaweza kutwaa ubingwa wa Epl katika mchezo dhidi ya Crystal Palace, Machi 20, lakini  Klopp anaamni ili wakamilikishe hilo  wachezaji wake hawapaswi kubweteka.

Jurgen Klopp amewaongoza majogoo wa Jiji Livepool kuweka Historia  ya kuibuka na ushindi katika michezo 18 mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wagonga nyundo wa London, West Ham United.

Kipindi cha pili cha mchezo huo wakiwa nyumbani Anfield kilitosha kupindua matokeo kutoka kuongozwa kwa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United na matokeo kuwa ushindi kwa Liverpool wa mabao 3-2.
 
Kwa sasa wanahitaji pointi 12 tu kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu England katika michezo 11 iliyosalia , Liverpool wameibuka na ushindi katika michezo 26 kati ya 27 waliyocheza hadi sasa.


Ushindi  dhidi ya West Ham United, unamaana kuwa wameifikia rekodi ya  Manchester City ya kuibuka ushindi katika michezo mingi zaidi (18) ya Epl  mfululizo, walifanya hivyo msimu wa 2017-18.

Ikiwa  Liverpool wataendelea kucheza kwenye kiwango chao, basi wanaweza kutwaa ubingwa wa Epl katika mchezo dhidi ya Crystal Palace, Machi 20, lakini  Klopp anaamni ili wakamilikishe hilo  wachezaji wake hawapaswi kubweteka.

"Sikuwa hata na matarajio kuwa tutaivunja au kuifikia (rekodi),’  alisema  Klopp, ambaye alishuhudia Mohamed Salah na  Sadio Mane wakiiokoa siku yake mbele ya West Ham.

" Tumefanya na siamini kama imewezekana kiukweli kabisa. Kila ambacho kimekuwa kikitokea ni juhudi za kila mmoja kwenye klabu."

Pamoja na kuwa West Ham ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1 kabla ya Salah na Mane kupindu matokeo, vijana hao wa David Moyes  kilichowagharimu katika mchezo huo ni makosa ya wa wachezaji binafsi