Liverpool yazidi kuwasha moto EPL

Muktasari:

  • Magori yaliyofungwa na Mohamed Salah dakika 38 na 90 yameifanya klabu hiyo kuzidi kujikita kileleni wakiwa na pointi 49 katika michezo 17 waliyocheza mpaka hivi sasa.

TIMU ya Liverpool imezidi kujiimarisha kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Watford, mchezo uliopigwa Uwanja wa Anfield.
Magori yaliyofungwa na Mohamed Salah dakika 38 na 90 yameifanya timu hiyo kujikita kileleni wakiwa na pointi 49 katika michezo 17 waliyocheza mpaka hivi sasa.
Huku Leicester City wanaoshika nafasi ya pili wao wana pointi 38 katika michezo 16 waliyocheza na hata wakipata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Norwich hawatoweza kuifikia Liverpool.
Liverpool imekuwa na ushindi mfululizo baada ya kushinda mechi zake tano za mwisho sawa na Leicester City ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo.
Desemba 26 Leicester watakuwa na kibarua kizito na Liverpool katika mchezo wao ambao utakuwa unampunguzia mmojawapo mbio za kuwania ubingwa.