Liverpool, City kimeeleweka

Muktasari:

Manchester City haijawahi kuondoka na ushindi Anfield katika mechi 17 za michuano mbali mbali walizocheza. Timu hiyo imewahi kupata ushindi mara moja Anfield mwaka 2003 iliposhinda 2-1

DAKIKA 45 KIPINDI CHA KWANZA

>Mechi imeanza...

>Dakika ya 2' mabao 0-0

>Dakika ya 10' mabao 0-0

>Dakika 45 mabao 0-0

Kipindi cha pili dak 45

> Liverpool 0-0 Man City dakika ya 50'

Manchester, England. Kocha Pep Guardiola, amekiongoza kikosi chake cha Manchester City  kwenye dimba la Anfield, baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana.

City bingwa ilikuwa na kazi nzito ya kulinda rekodi yake ya ushindi kwa msimu huu mbele ya Liverpool ambayo haifungiki kirahisi kwenye dimba lao la nyumbani.

Hilo lilimfanya Guardiola, kuingiwa na woga wakati akijiandaa kwa mchezo huo, akisema kucheza kwenye uwanja wa Anfield ni sawa na kucheza kwenye uwanja wa vita.

Awali alisema, “Ninapafahamu vizuri Anfield ni bahati kupata japo pointi moja, msimu uliopita tulifungwa mabao 4-3, tulikuwa na wakati mgumu sana na hata katika Ligi ya Mabingwa Ulaya tulifungwa 3-0, hakika Anfield ni uwanja mgumu sana kupata pointi,” alisema.

Guardiola alisema alijua ugumu wa uwanja huo kwa City haujaanzia kwake bali hata makocha waliomtangulia walipata tabu, tangu ilipopata ushindi wa 2-1 mwaka 2003, kwa mabao ya Nicolas Anelka, Kocha huyo alikiri kuwa mbali ya ugumu wa uwanja kutokana na sapoti ya mashabiki lakini pia ubora wa kikosi cha sasa cha Liverpool hasa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Roberto Firmino, Mohamed Salah na Sadio Mane.

Kwa upande wake Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, alisema waliuchukulia mchezo huo kwa umakini mkubwa, wakijua ni kazi ngumu kuizuia City.

Majeruhi walioukosa mchezo huo kwa Liverpool ni kiungo, Alex Oxlade-Chamberlain wakati kwa City, itawakosa Ilkay Gundogan anayesumbuliwa na msuli, Fabian Delph na Claudio Bravo.