Liuzio aipania KCCA Afrika

Muktasari:

  • Akizungumzia na Mwanaspoti Liuzio alisema kombinesheni yao ni nzuri, na ni wazi wataisaidia timu yao katika mchezo huo wa ugenini na hata wa marudiano wiki mbili zijazo.

KIKOSI cha Mtibwa Sugar kilitarajiwa kuondoka asubuhi ya leo Alhamisi kwenda Uganda kwa mchezo wao wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KCCA ya Uganda, huku straika wao Juma Liuzio akila kiapo.

Liuzio alisema kombinesheni yake na Jaffar Kibaya iliweza kuzaa matunda dhidi ya Northen Dynamo ya Shelisheli na hadhani kama KCCA watashindwa kuwafunika jijini Kampala.

Liuzio na Kibaya ni wachezaji wenye nguvu, spidi na uwezo wa kupiga mashuti hali inayowasumbua mabeki wanaokutana nao katika Ligi Kuu mpaka katika michuano hiyo ya Shirikisho.

Akiizungumzia na Mwanaspoti Liuzio alisema kombinesheni yao ni nzuri, na ni wazi wataisaidia timu yao katika mchezo huo wa ugenini na hata wa marudiano wiki mbili zijazo.

“Tunaenda kwa lengo la kushinda kama kocha atatuanzisha pamoja naamini tutafanya kweli kwani mimi na Kibaya soka letu linaendana na kila mwana Mtibwa ana kiu ya kuona tunafika mbali,” alisema.

Liuzio alikiri mchezo wao na KCCA ni mgumu na kusisitiza ni lazima mabeki wao wajipange na kupata ushindi wa ugenini.