Lingard akomaa Manchester United akataa kwenda Arsenal

Muktasari:

Lingard anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake huko Man United na tyari ameonekana kufutwa kwenye mipango ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.

LONDON, ENGLAND. ARSENAL mpo? Jesse Lingard amesema kwamba atabaki Manchester United apiganie nafasi na hata kama atakaa benchi sio mbaya, lakini si kwenda kujiunga na Arsenal.
Kiungo huyo Mwingereza alisema kwamba hana mpango na wala hajawahi kushawishika na mpango wa kwenda kujiunga na Arsenal, ambao wamedaiwa wanahitaji saini yake wakati dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi litakapofunguliwa.
Lingard anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake huko Man United na tyari ameonekana kufutwa kwenye mipango ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.
Arsenal wanaripotiwa kwamnba wanahitaji kumpa Lingard sehemu ya kukimbilia, lakini taarifa zidai kwamba mchezaji huyo anadai kwamba ni heri abaki Man Unitd kugombea nafasi.
Kocha Solskjaer amedaiwa kwamba anajiandaa kuondoa wachezaji wa ziada kwenye kikosi chake ili kupata pesa za usajili, huku Pauni 30 milioni zinaripotiwa kwamba zitatosha kumng'oa Lingard kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.
Lingard, aliyeibukia kwenye akademia ya Man United amefunga mabao mawili tu katika mechi 35 alizocheza msimu huu.