Lineker atia neno uwezo alionyesha Samatta dhidi Liverpool -VIDEO

Muktasari:

Samatta alifunga bao hilo akiunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Junya Ito, lakini teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi 'VAR', ilikataa bao hilo ikionyesha Ito alikuwa amezidi kidogo sana wakati akipokea mpira kabla ya kupiga krosi.

Dar es Salaam.Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England, klabu ya Barcelona, Gary Lineker ameshangazwa na uamuzi wa kukataliwa kwa bao la mshambuliaji Mbwana Samatta katika mchezo wa jana wa Ligi ya Mabingwa kati ya Genk na Liverpool.

Lineker aliyekuwa mchambuzi katika mchezo huo aliandika katika ukurasa wake wa Twitter@GaryLineker

What Samatta with that? na kupata Retweets 474 na Likes 4.5K pamoja na maoni 394 kutoka kwa watu mbalimbali wanaofuata katika mtandao huo.

Wakati Liverpool wakiwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Oxlade-Chamberlain, Samatta alifunga bao, ambalo lingekuwa la kusawazisha kwa kichwa katika kipindi hicho cha kwanza, lakini mwamuzi wa mchezo huo, Slavko Vincic aliomba usaidizi wa VAR.

Samatta alifunga bao hilo akiunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Junya Ito, lakini teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi 'VAR', ilikataa bao hilo ikionyesha Ito alikuwa amezidi kidogo sana wakati akipokea mpira kabla ya kupiga krosi.

Baada ya kutazamwa bao lile la Samatta, Mslovenia ambaye alikuwa akichezesha mchezo huo, alilikataa huku wengine wakidhani kuwa kumtuia kwake James Milner kama ngazi ilichangia na wengine wakiliona tukio lile kuwa huenda alikuwa kwenye eneo la kuotea.

Baada ya kukataliwa kwa bao hilo mashabiki wa Genk 20, 000 waliokuwa uwanjani hao walipiga kwa kumzomea mwamuzi kwa kukataa goli hilo.

Hali hiyo iliyokuwa uwanjani ndiyo ilivyokuwa Tanzania nyumbani kwa Samatta, ambako kwao bao hilo lilikuwa na umuhimu wa kipekee, liliripoti gazeti la The Sun la England.