Ligi Kuu yamtisha kipa Alliance FC

Muktasari:

Mwanda alisema bado hawako nafasi mbaya kwenye ligi lakini wanatakiwa kupambana ipasavyo ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwa kila mchezo watakaocheza.

KIPA wa Alliance FC, John Mwanda ameangalia msimamo wao kwenye Ligi Kuu kisha akawaambia nyota wenzake wa kikosi hicho kuwa wanatakiwa kupambana ipasavyo ili kukaa nafasi nzuri na kukwepa kushuka daraja msimu ujao.
Mpaka sasa Alliance wanashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi huku wakiwa na pointi 17  wakicheza mechi 13.
Mwanda alisema bado hawako nafasi mbaya kwenye ligi lakini wanatakiwa kupambana ipasavyo ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwa kila mchezo watakaocheza.
“Ligi imekuwa ngumu sana msimu huu tunachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha tunapambana vya kutosha kila mchezo tutakaocheza kupata matokeo mazuri ambayo yatatuweka salama na janga la kutokushuka daraja,”
“Japo hatupo nafasi mbaya sana lakini tunahitaji kujituma zaidi ili angalau ligi itapomalizika tuwe nafasi tano za juu niwaombe mashabiki waendelee kutupa ushirikiano kwani tunahitaji sana nguvu zao kufanikisha malengo haya,”alisema Mwanda