Ligi 6 bora duniani zafikia patamu!

Muktasari:

  • Tathmini inaonyesha kwamba mpaka sasa wachezaji wanaoongoza kwa ufungaji wa mabao hayazidi 11 ingawa kuna nafasi ya kufanya vizuri kwa kadri siku zinavyoendelea.

London, England. Duniani kuna ligi kibao, lakini kwa taarifa yako ni kwamba ligi ambazo zinafuatiliwa kwa karibu ni tano. Yaani ile ya England, Hispania, Ujerumani, Italia na Ufaransa.

Taarifa nyingine ni kwamba, mpaka kufikia sasa ligi nyingi kati ya hizo zimeshacheza mechi zaidi ya 10 katika mzunguko wa kwanza wa msimu wa 2018/19.

Katika mzunguko huu wa kwanza kuna maajabu yanaendelea, kuna ukweli usiopingika kwamba kuna wachezaji, ambao walikuwa wakitegemewa kuwa vinara katika upachikaji wa mabao katika ligi hizo. Hata hivyo, wamekwama kidogo kutokana na ushindani mkubwa, huku sura kadhaa mpya (si zote) zikionekana kutikisa dunia katika zoezi zima la ufungaji kwa sasa.

Tathmini inaonyesha kwamba mpaka sasa wachezaji wanaoongoza kwa ufungaji wa mabao hayazidi 11 ingawa kuna nafasi ya kufanya vizuri kwa kadri siku zinavyoendelea.

Kwa makala zaidi za uchambuzi usikose nakala ya Gazeti lako la Mwanaspoti.