Leseni ya Shikalo tayari, Molinga bado

Muktasari:

Mwakalebela amesema leseni za wachezaji wengine wawili David Molinga na Mustapha Seleman wanaendeleza kuzifuatilia.

KIPA namba Moja wa Yanga, Farouk Shikalo ruksa kuanza kuIchezea timu hiyo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United baada ya leseni yake kutua.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema tayari wamepata leseni ya Shikalo na uamuzi wa kucheza mchezo huo utakaofanyika Septemba 14 unabaki kwa kocha Mwinyi Zahera.
Mwakalebela amesema leseni za wachezaji wengine wawili David Molinga na Mustapha Seleman wanaendeleza kuzifuatilia.
Shikalo aliyesajiliwa na Yanga kutoka Bandari FC ya Kenya alishindwa  kuichezea timu yake mechi dhidi ya Township Rollers kutokana na kukosa leseni hivyo  taarifa hii inaweza kuwa furaha kwake na kwa Zahera.