Leopards yakiri Simba mziki mnene

Friday January 25 2019

 

By THOMAS NG’ITU

KOCHA  wa AFC Leopards ‘Ingwe’ ya Kenya, Marko Vasiljevic
amekiri kwamba ‘mziki’ wa Simba ni habari nyingine kwao.
Simba na Leopards walikutana katika mchezo wa Kombe la Sportpesa hatua ya makundi  ambapo Leopards walikubali kichapo cha mabao 2-1 na kutolewa kwenye mashindano hayo.
Akizungungumza na Mwanaspoti, Marko alisema uwezo wa Simba hivi sasa ni mkubwa kutokana na kucheza mashindano makubwa na kukutana na timu mkubwa.
“Mimi mwenyewe ni mzoefu wa mashindano makubwa kwahiyo ninapokutana na timu ambayo inacheza mashindano hayo na kukutana na timu kama As Vital na Al Ahly unatakiwa uiheshimu, kikubwa naamini vijana wangu wamepata uzoefu zaidi,” alisema.
Marko aliongeza kwamba katika mchezo huo vijana wake
wamejitahidi lakini makosa madogo madogo ndio yamewagharimu.
“Tulicheza vizuri lakini baadaye tulifanya makosa ndio maana
nikafanya mabadiliko, baada ya mabadiliko kila mmoja aliona
tuliwashambulia, hatuna jinsi hivi sasa tunaangalia ligi yetu ya
nyumbani,” alisema.

Advertisement