Lema humwambii kitu kwa Lakers

Monday July 15 2019

 

By Eliya Solomon

KILA mtu anakuwa na mapenzi yake hasa linapofika suala la michezomingine mbalimbali nje ya soka ambao ni kipenzi cha mabashabiki wengi.

Kwa kinda wa Kitanzania, Michael Lema anayeichezea SK Sturm Graz ya Austria, amefichua yeye ni mnazi wa kutupwa wa timu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Lakers ya Marekani.

Lema alisema pamoja na ukata uliopo Los Angeles Lakers, ipo siku watarejea kwenye furaha kama ilivyokuwa kwenye miaka ya 2009 na 2010.

Kinda huyo, alisema mapenzi yake ya mchezo wa mpira wa kikapu ni makubwa na amekuwa akifuatilia Ligi ya Kikapu ya Marekani maarufu kama NBA kwa miaka mingi.

“Navutiwa na mpira wa kikapu, wapo ambao wanaichukulia poa Lakers lakini ipo siku itakuja kutawala tena NBA kwa miaka mfululizo,” alisema

Lakers imetwaa mataji 16 ya NBA kwenye miaka ya 1949, 1950, 1952, 1953, 1954, 1972, 1980, 1982, 1985, 1987, 1988, 2000, 2001, 2002, 2009 na 2010.

Advertisement

Miamba hiyo ya Marekani, inashikilia rekodi ya kuwa timu pekee iliyoibuka na ushindi kwenye michezo mingi ya NBA ambayo ni 33, waliyoiweka kuanzia mwaka 1971 hadi 1972.

Advertisement