Lampard kuisuka upya Chelsea, amtaka Zaha

Muktasari:

Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema anataka kuisuka timu hiyo kwa kusajili wachezaji mahiri akiwemo nyota wa Crystal Palace Wilfried Zaha.

London, England. Chelsea inatarajia kuvunja benki kufanya usajili wa nguvu katika dirisha dogo Januari, mwakani.

Kocha Frank Lampard ameandaa fungu kubwa la usajili na miongoni mwa nyota anaowataka ni mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha.

Hata hivyo, Chelsea itazimika kusubiri pingamizi lake ililotuma kupinga adhabu ya kufungiwa kutofanya usajili.

Chelsea ilikumbana na rungu la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kosa la kusajili wachezaji wenye umri mdogo na nyota wa kigeni, hivyo atakuwa na ruska ya kusajili hadi majira ya kiangazi

Klabu hiyo imetenga Pauni150 milioni kunasa saini za mastaa wapya akiwemo mchezaji huyo katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwakani.

Pia Lampard anataka saini ya beki wa kushoto wa England Ben Chilwell ambaye amekuwa na kiwango bora Leicester City.

“Siku zote Chelsea tumekuwa na ndoto ya kupenda mafanikio, tukipata ruska ya kusajili tutaangalia wachezaji bora ambao watakuja kuimarisha kikosi chetu,”alisema Lampard.

Chelsea ina fedha baada ya kumuuza aliyekuwa nyota wake Edin Hazard kwenda Real Madrid katika usajili wa majira ya kiangazi msimu uliopita.

&&&&&&&&&