Lampard awashushia lawama waamuzi

Sunday October 25 2020
lampard pic

MANCHESTER, ENGLAND. KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard anaamini timu yake ilistahili  kupewa penalti  wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya  Manchester United  kutokana na faulo ambayo Harry Maguire  alimchezea beki wake  Cesar Azpilicueta.

Nahodha wa The Blues, Azpilicueta alikabwa shingoni na Harry Maguire kwenye mchezo huo ambao uliomalizika suluhu (0-0).

Tukio  hilo  ambalo lilitokea baada ya kuchongwa kwa kona, lilirejewa na teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi 'VAR' lakini haikubainika kuwa  Maguire  alifanya faulo.

"Ni wazi kuwa sikuliona vizuri  tukio wakati likitokea kutokana na mahali niliposimama. Wao pia ni ngumu kuona kwa haraka ilihitaji waamuzi kwenye uwanja kufanya maamuzi, lakini VAR ilitumia muda mchache kulitazama kwa makini tukio ni maoni yangu.

"Nadhani walipaswa kuchukua muda na kumshauri mwamuzi aangalie kwa umakini juu ya kilichotokea.Endapo mwamuzi angeenda kufuatilia basi angetoa adhabu," amesema.

Manchester United, ambao wameendelea kukwama kati ya timu 10 za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, matokeo ya mchezo huo yamewafanya kutopoteza michezo mitatu mfululizo ya mwanzoni mwa msimu wakiwa nyumbani kwa mara ya kwanza tangu 1930.

Advertisement

Aliyekuwa shujaa kwa Chelsea kwenye mchezo huo alikuwa mlindalango wao Edouard Mendy, ambaye aliokoea michomo mitatu ya hatari, ikiwemo miwili ya Marcus Rashford, ikiwemo moja ambayo ilikuwa ya dakika za mwishoni kabisa kabla ya mchezo kumalizika.

Katika mchezo huo pia alishuhudiwa Edinson Cavani, akiichezea Manchester United mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo, aliingia kipindi cha pili sambamba na Paul Pogba.

Wakati huo huo, kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer alizungumzia tukio la Maguire, Azpilicueta kwa kusema, "Sio vibaya kuchukua nafasi. Kijana huyo alimnasa tu na Harry labda haikufaa kuweka mikono yake karibu naye, alichofanya ni kuondoa hatari tu," amesema.

 

Advertisement