LIVE>>VIDEO: Jonas Mkude aongoza jahazi msafara Simba

Saturday January 12 2019

By OLIPA ASSA

Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ndiye alikuwa  wa kwanza kukiongoza kikosi cha Simba kushuka kwenye gari baada ya gari la timu  hiyo kutua Uwanja wa Taifa 2:26.

Simba wanaanza kutupa karata yao ya kwanza leo Jumamosi hatua ya makundi ya Ligi ya  Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura, mchezo unapigwa saa 10:00 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mashabiki hawapo nyuma wanaendelea kufurika kuiunga mkono timu yao, huku wakiwa na matumaini  makubwa Simba kuchomoza na ushindi mnono.

Wakati mashabiki wakiendelea na shamrashamra zao, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Suma JKT hawapo nyuma kuhakikisha usalama wa raia unakuwa sawa sambamba na kuwaelekeza sehemu za kukaa kutokana na bei za tiketi zao.

Advertisement