Kylian Mbappe, Ronaldo sasa unaanzaje kununa

PARIS, UFARANSA. SUPASTAA, Cristiano Ronaldo amejibu posti ya Kylian Mbappe aliyotuma kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya wawili hao kukutana kwenye mchezo wa Nations League.

Fowadi hao, hakuna hata mmoja aliyefunga mabao kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 0-0, kuzifanya Ufaransa na Ureno kulingana kwa pointi kwenye League A Kundi 3 zikiwa na pointi saba.

Mechi hiyo ilikuwa siku muhimu kwa Mbappe, ambaye alifichua kwamba amekuwa akimfuatilia fowadi huyo wa Juventus na kujaribu anachokifanya kwa muda wote wa makuzi yake.

Baada ya mechi, straika wa PSG alimtumia meseji Ronaldo kwenye Insta, aliposhea picha inayowaonyesha wawili hao wakiwa pamoja uwanjani na kuandika neno moja tu “idol” kisha akaweka picha ya taji na emoji ya mbuzi. Ronaldo naye alimjibu kwa emoji.

Wawili hao walionekana kuwa na wakati mzuri uwanjani, ambapo walionekana wakicheka kabla ya kupindi cha pili kuanza.

Ronaldo alimnong’oneza sikioni Mbappe na kisha akapiga kichwani na baada ya hapo, wawili hao kila mmoja alionekana akicheka. Walikumbatiana pia baada ya mechi kumalizika.

Mbappe, ambaye amefunga mabao 15 katika mechi 37 alizochezea timu yake ya taifa, umri wake wa miaka 21 na amewahi kuzungumza namna anavyomkubali Ronaldo.

“Yeye ni shujaa wangu wa tangu utoto na ilikuwa jambo zuri kukutana naye wakali nilipotembelea Valdebebas,” alisema Mbappe.