Kwa Arsenal hii mtapata tabu sana

Muktasari:

Kocha wa Arsenal Unai Emery, aliyeanza ligi kwa kupoteza mechi mbili mfululizo, sasa ameendelea kupata matokeo bora yanayowaduwaza wengi baada wa jana kuiadhibu Leicester City kwa mabao 3-1 na kupanda hadi nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa pointi mbili tu nyuma ya vinara Manchester City na Liverpool, baada ya kila timu kuche mechi tisa.

London, England. Mashabiki wa Arsenal sasa roho kwatu kabisa wanafurahia matokeo ile mbaya chini ya kocha wao Unai Emery jana alishudia timu yake ikishinda mchezo wa kumi mfululizo ilipoichapa kwa mabao 3-1 Leicester City.

Ushindi huo umemfanya kocha Emery kuwa shujaa na sasa anaamiwa vilivyo na mashabiki wakiamini amestahili kukaa kwenye nafasi ya Arsene Wenger aliyeiongoza timu hiyo kwa zaidi ya miaka 20 kabla ya kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita.

Emery alianza ligi kwa kupoteza mechi mbili za kwanza dhidi ya Manchester City na Chelsea na kuzusha hofu, lakini baada ya hapo ameshinda mechi zote saba zilizofuata na sasa yupo sawa kwa pointi na Chelsea ambayo haijapoteza hata mechi moja, lakini imetoa sare mechi tatu.

Kocha huyo anazidi kujipatia uungwaji mkono mkubwa na mashabiki na hili linathibitishwa na mahudhurio ya mashabiki katika mechi za nyumbani kwenye dimba la Emirates unaochukua watazamaji 60,000.

Katika mchezo wa juzi Arsenal ilitangulia kufungwa baada ya mlinzi wake Hector Bellerin kujifunga alipobabatizwa na shuti la Ben Chilwell, akiipa Leicester bao la kuongoza lakini Mesut Ozil alisawazisha dakika ya 45 na kwenda mapumziko zikiwa 1-1.

Katika kipindi cha pili Arsenal iliongeza mashambulizi kwa kuingia akitokea benchi Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gabon alithibitisha ubora wake baada ya kuifungia mabao mawili dakika ya 63 na 66 ushindi uliopaisha hadi nafasi ya nne katika msimamo.

Mchezo huo ulishuhudiwa na kocha wa zamani wa timu hiyo Arsene Wenger, ambaye alikuwa akisherehekea miaka 69 ya kuzaliwa kwake.

Katika mchezo huo kocha Emery alimuanzisha Matteo Guendouzi katika kiungo huku akimchezesha pembeni kushoto kiungo mwenye nguvu wa Uswisi, Granit Xhaka.