Kwa 20% ni akili na mipango tu

Muktasari:

Mashabiki wengi wa mwanamuziki wa bongo fleva, 20 Pacent wamekuwa wakijiuliza nini kimempata staa huyo baada ya kimya kingi, amejibu na kuwataarifu kwamba anarejea kwa kishindo.

HAKUNA ubishi kwamba Abbas Hamis '20 Pacent' enzi akitamba aliacha alama nyingi kwenye muziki wa kizazi kipya kabla ya kuwa kimya kwa muda mrefu, lakini unaambiwa sasa jamaa anakuja kivingine.
20 Pacent amefichua wengi wanadhani jamaa kafulia ndio maana hasikiki, ila ukweli ni kwamba amekuwa akitoa nyingi nyingi lakini hazina video hivyo ngumu mashabiki wake kushindwa kumuona kama walivyozoea miaka ya nyuma.
Amesema moja ya kazi hizo ni Jieleze na msanii huyo amesema ataachia video ya nyimbo mbili ambazo ni Misukosuko na Wema Usizidi Uwezo, akidai ndani yake kuna majibu mengi ya maswali ya mashabiki wake.
"Labda kitu wasichojua mashabiki kutoka kwangu, nikirejea nitatumia akili na sio nguvu kubwa, wasanii wanaotamba kwa sasa wanatumia nguvu nyingi ili kutuzika ila sidhani kama watafanya hivyo mpaka mwisho.
"Mbali na nyimbo nimefanya filamu tisa, nne zinahusu maisha yangu ya muziki na tano maisha ya kawaida ya uhalisia wa Mtanzania, nakuja kwa kishindo kitakachotikisa wengi.
"Nitaanza kutoa filamu ya maisha ya kawaida ya Watanzania badae nitatoa kuhusu mziki wangu, hivyo nitavifanya mwezi Desemba, ili kuhusu nyimbo zangu ambazo ni misukosuko na wema usizidi uwezo nitazitoa ndani ya mwizi huu,"anasema.