Kumbe tatizo ni mameneja!

Muktasari:

  • Kitendo cha wachezaji kuonekana kuwa na matatizo hasa ya utovu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja ni kutokana na kukosa mameneja wa kuwaongoza nyota hao. Hilo limefanyiwa uchunguzi na makocha mbalimbali wa soka na kupata majibu hayo.

MASHABIKI wa soka wamekuwa wakitupia lawama nyota mbalimbali wa soka hasa waliobobea kwenye matukio ya utovu wa nidhamu, lakini imeelezwa linalochangia wachezaji hao kuwa hivyo ni kukosa mameneja wazuri wa kuwaongoza.

Makocha mbalimbali wa klabu za soka nchini, wamesema wachezaji wakiwa na mameneja wa wakuwaongoza na kuwasimamia ndani na nje ya uwanjani ni wazi itasaidia kuwashepu vyema kama wachezaji wa kulipwa, tofauti na ilivyo sasa.

Kocha wa Mbao, Amri Said, alisema ili nidhamu iwe kubwa kwa wachezaji lazima mameneja wanaowasimamia wawajibike kwa asilimia 100.

“Meneja wa mchezaji lazima awe wa kwanza kuangalia soko la mteja wake ambalo lina vipengele kama nidhamu ndani na nje ya uwanja, kiwango chake kinasababishwa na nini kuwa juu ama kinashushwa na nini.

Naye Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilal ‘Bilo’ alisema soka lina vipengele vyake ambavyo vikiungana kwa pamoja vinaweza kubadili taswira na kuwa kimataifa zaidi.

“Kocha ana sehemu yake kwa mchezaji, yupo meneja anayepaswa kulinda biashara iwe na manufaa lakini wanaonekana kuwa nyuma. Kwanza meneja ndiye anakuwa anajua fika tabia ya mteja wake hivyo anapaswa kumfuatilia kila anachofanya,” alisema Bilo.

Kocha wa Prisons iliyotoka kugongwa mabao 2-1 na Mbeya City juzi jijini Mbela Abdallah Mohammed ‘Bares’ kwa upande wake alisema meneja wa mchezaji anapaswa kuwa mshauri mzuri na kukemea pale anapoona mteja wake anakiuka suala la nidhamu.

“Kocha lazima awajibike kwa kumfanya mchezaji awe na kiwango lakini pia meneja ana nafasi kubwa.”