Kumbe mashabiki wa Simba waliitishia Nyau Gor Mahia

Friday June 8 2018

By Fadhili Athumani

 Nakuru. Umewahi kuona mwanamume akitishiwa nyau nyumbani kwake, tena mbele ya mke na watoto wake?  Kuna watu wana kiburi katika hii dunia lakini kiburi cha mashabiki wa Simba kimezidi aisee. Sikia hii

Wakati joto la mchezo wa fainali ya Sportpesa Super Cup, utakaokutanisha mafahali wawili katika soka la Afrika Mashariki, mabingwa watetezi Gor Mahia na mabingwa wa soka nchini Tanzania, Simba SC,  ukiendelea kushika kasi, Mwanaspoti imenyetishwa kuwa, mashabiki wa Simba wameamua kuwatishia Kogalo nyau.

Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, ni kwamba, katika mchezo wa nusu fainali ya pili, iliyoshuhudia Gor Mahia ikiwabandua Singida United, mashabiki wa Simba waliofurika katika uwanja wa Afraha, mjini Nakuru, walikuwa na kazi moja tu, kuwazomea mashabiki wa Kogalo.
Taarifa hizo zinasema kuwa, wakiwa wanajiamini, mashabiko hao, maarudu wekundu wa msimbazi, wakiwa wametinga jezi zao nyekundu, walionekan wakiimba huku wakiwaoneshea mashabiki wa Gor Mahia ishara ya kukata shingo wakimaanisha kuwa wajiandae kuchinjwa siku ya Jumapili watakapokutana
Baada ya kuwazima Kakamega Homeboyz, ambao ni wababe wa Yanga, Simba inaamini kombe hilo ni lao na hili walilithibitisha katika nyimbo zao kwenye dimba la Afraha. Katika nyimbo wekundu hao walisikika wakiimba:
“Tuko hapa kumbeba mwali, Sportpesa ni yetu, sisi ndio Simba, Simba ni ni mmoja tu Afrika Mashariki  na hatishwi na yeyote. Sisi ndio wafalme wa Porini, hili ni pori letu, hatutishwi, mtayarishe mifuko ya kubebea magoli"
Hata hivyo, mashabiki wa Gor Mahia ambao ndio kwanza walikuwa wanashingilia bao la ushindi la Meddie Kagere anayewindwa na Yanga, wakiongozwa na Bishop Sudi Jaimbo, waliwageukia wana msimbazi hao na kuanza kuwazomea, wakisema:
“Haoo hamna lolote mlipita kwa penalti, hakuna goli hata moja, mtawezaje kuifunga 'mighty Kogalo' ati timu bora Afrika mashariki, sisi ndio Kogalo, sisi ndio 'chuor timbe' (mabwana wa vilabu), tutawaonesha mchezo unavyochezwa. Tutawapiga vilivyo"
Mechi ya fainali, itanguruma siku ya Jumapili, Juni 10, katika uwanja wa Afraha ambapo mshindi wa makala ya pili ya Sportpesa Super Cup, ataondoka na kitita cha shilingi milioni 3 (sawa na Tsh60 milioni), Kombe na fursa ya kwenda Goodison Park, nchini Uingereza kucheza na Everton FC. 

Nakuru. Umewahi kuona mwanamume akitishiwa nyau nyumbani kwake, tena mbele ya mke na watoto wake?  Kuna watu wana kiburi katika hii dunia lakini kiburi cha mashabiki wa Simba kimezidi aisee. Sikia hii
Wakati joto la mchezo wa fainali ya Sportpesa Super Cup, utakaokutanisha mafahali wawili katika soka la Afrika Mashariki, mabingwa watetezi Gor Mahia na mabingwa wa soka nchini Tanzania, Simba SC,  ukiendelea kushika kasi, Mwanaspoti imenyetishwa kuwa, mashabiki wa Simba wameamua kuwatishia Kogalo nyau.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, ni kwamba, katika mchezo wa nusu fainali ya pili, iliyoshuhudia Gor Mahia ikiwabandua Singida United, mashabiki wa Simba waliofurika katika uwanja wa Afraha, mjini Nakuru, walikuwa na kazi moja tu, kuwazomea mashabiki wa Kogalo.
Taarifa hizo zinasema kuwa, wakiwa wanajiamini, mashabiko hao, maarudu wekundu wa msimbazi, wakiwa wametinga jezi zao nyekundu, walionekan wakiimba huku wakiwaoneshea mashabiki wa Gor Mahia ishara ya kukata shingo wakimaanisha kuwa wajiandae kuchinjwa siku ya Jumapili watakapokutana.

Advertisement