Kumbe Bocco alikaushiwa Yanga

Muktasari:

· Katika hatua nyingine, kiungo fundi wa Yanga, Mzimbabwe Thabani Kumusoko, amerudishwa katika kikosi chake cha timu ya taifa baada ya ufundi wake akiwa na Yanga kufika nchini kwao.

YANGA ililetewa jina la nahodha wa Azam, John Bocco, lakini usajili wake usingeweza kukamilika baada ya kocha, George Lwandamina, kumkaushia kwa madai kwamba si aina ya wachezaji anaowataka.

Bocco maarufu kama Adebayor, amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba huku kipa Aishi Manula akitajwa kumfuata kutokana na mpango mpya wa Azam kubana matumizi.

“Uongozi hausajili, anayesajili ni kocha mkuu na wasaidizi wake, wakituletea huku kwetu tunachofanya ni kumalizia maongezi na kuingia mikataba sasa Bocco ni kweli tuliambiwa yuko huru na wanataka aje hapa lakini kocha wetu hakuonyesha kumhitaji,”alisema mmoja wa viongozi wa usajili wa Yanga.

Katika hatua nyingine, kiungo fundi wa Yanga, Mzimbabwe Thabani Kumusoko, amerudishwa katika kikosi chake cha timu ya taifa baada ya ufundi wake akiwa na Yanga kufika nchini kwao.

Mara baada ya kumaliza mechi ya mwisho wa ligi, Yanga imepokea mwaliko wa Kamusoko akiitwa katika kikosi cha wachezaji 23 waliotajwa kuingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki.