Kulialia agoma kurudi Akudo Impact -VIDEO

Muktasari:

Mwanamuziki Fabrice Kulialia amesema hana mpango wa kurudi bendi ya Akudo Impact kutokana na kupata mdhamini wa bendi yake East Africa Ngwasuma iliyopo Arusha jijini.

KAMA unadhani mwanamuziki wa kongo Fabrice Kinyenya 'Kulialia' ana mpango wa kurudi Akudo Impact pindi itakapokuwa hai, basi ondoa hilo wazo.


Mwimbaji huyo aliyepojijini Arusha akiipigia bendi ya East Africa Ngwasuma akiwa kiongozi amesema hana mpango wa kurudi Akudo kwani tayari anamiliki bendi ambayo inaenda vizuri katika muziki wa dansi.


"Kiukweli siko tayari kurudi Akudo Impact hata kama itafufuka sasa hivi katika ulimwengu wa dansi, nina bendi jijini Arusha na nina mdhamini anayesababisha mambo mazuri hivyo siwezi kuacha haitakuwa vizuri," amesema Kulialia


Aidha Fabrice aliyekiri Akudo ndio iliyomleta Tanzania na wimbo wa kwanza kuimba ilikuwa ni 'Msaliti' alishirikishwa na Christian Bella amesema, aliondoka Akudo sababu hakukuwa na matunda wa kile wanachokifanya kwani walikuwa wanazalisha bila.


Hata hivyo, amesema ana nyimbo zake nyingi zipo mtandao wa Youtube Channel yake zikiwemo 'Umaskini' na 'Maumivu ya Mapenzi' na hata hivyo wapo katika maandalizi ya kutoa nyimbo za bendi.


Fabrice amesema kwa sasa Arusha na maeneo ya karibu wameanza kuupenda muziki  wa dansi na alipoulizwa na MCL Digital juu ya kuibuka kwa waimbaji wanaojipa majina mbalimbali kama Mfalme wa Masauti, Mfalme wa Rhumba,kwake vipi naye alisema  hawezi kujiita Mfalme bali anafahamika kama Kiboko wa Masauti.

4
Bendi ya Akudo 'Wazee wa Masauti' iliwahi  kutamba na mtindo wa Pekechapekecha ilikuwa inaundwa na wanamuziki Christian Bella,Tarsis Masela, Kanal Top, Allan Kabasele na wengineo.