Kuiona Azam FC, Triangle United buku tatu tu

Thursday September 12 2019

 

By Yohana Challe

Dar es Salaam. Mashabiki wa AzamFC wataishuhudia mechi mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle United FC ya Zimbabwe kwa kiingilio cha Sh3,000 na Sh 10,000 kwa VIP kwenye Uwanja wa Chamazi Complex.

Tiketi zitaanza za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho Ijumaa katika vituo vya Dar Live, Chamazi Complex, kwenye duka la Ice Cream, na pale Azam Shop.

Afisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd alisema mchezo huo ni muhimu kwa timu zote mbili hasa katika kusaka nafasi ya kujiweka vyema wanapopata matokeo mazuri katika mchezo huo.

"Hii ni nafasi nyingine kwa Watanzania kuisapoti timu yao ili izidi kupeperusha bendera ya taifa katika mashindano hayo," alisema Idd.

Azam inayonolewa na Kocha Etienne Ndayiragije imekuwa na matokeo mazuri zaidi inapocheza uwanja wake wa nyumbani kuliko ugenini hivyo rekodi hiyo inaonekana kuwabeba kuelekea katika mchezo huo wa Jumapili.

Ndayiragije na vijana wake walifanikiwa kutinga hatua hiyo kwa kuitoa Fasil Kenema ya Ethiopia kwa uwiano wa mabao 3-2 baada ya ushidi wa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Chamazi Complex huku katika mchezo wa kwanza wakikubali kulala kwa bao 1-0, wakati wapinzani wao wakiitoa Rukinzo FC ya Burundi kwa jumla ya mabao 5-0 baada ya suluhu katika mchezo wa mwisho.

Advertisement

 

Advertisement