Kozi ya kimataifa ya kuogelea yaanza

Friday January 12 2018

 

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Kozi ya kimataifa ya waamuzi wa kuogelea imeanza leo jijini Dar es Salaam ambayo inaendeshwa na mkufunzi kutoka Nigeria.

Kliniki hiyo imeanza leo Januari 12 jijini Dar es Salaam hadi Januari 14.

 Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka amesema kliniki hiyo inaendeshwa na mkufunzi kutoka Nigeria, Olugbenga Akinsanya Lawal.

Lawal ni mjumbe wa kamati ya ufundi ya Shirikisho la Mchezo wa kuogelea la Afrika (CANA) na pia aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya ufundi ya Shirikisho la Kimataifa la Mchezo wa Kuogelea (FINA).

Namkoveka aliongeza kuwa waamuzi 40 wanatarajiwa kushiriki kwenye kliniki hiyo na wale watakaofuzu watapata nafasi ya kuwa waamuzi wa kimataifa.

Kliniki ya waamuzi hao lengo kuu ni kuendeleza na kukuza kiwango cha mchezo wa kuogelea na kuimarisha ubora wa waamuzi.