Koeman kukomaa na wawili Barca

BARCELONA, ENGLAND. PALE England msimu ujao kutakuwa na shughuli kubwa kati ya Barcelona na baadhi ya klabu ambazo zina wachezaji wanaotakiwa na wababe hao wa Hispania.

Ripoti zinadai Barcelona inajiandaa kukamilisha usajili wa wachezaji wawili ambao ni kiungo wa Liverpool, Gini Wijnaldum na beki wa Manchester City, Eric Garcia katika dirisha hilo la mwezi Januari.

Wachezaji hao watakuwa huru katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi lakini Koeman anataka kufanikisha usajili wao katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

kocha wa wababe hao, Ronald Koeman aliutaka uongozi wa timu hiyo kuhakikisha unaipata saini ya Wijnaldum ambaye aliwahi kumfundisha katika timu ya Taifa ya Uholanzi na Garcia aliyelelewa hapo katika timu za vijana, lakini madili hayo yalifeli.

Barca ambayo imepata hasara ya Pauni 88 milioni kwa msimu uliopita kutokana na janga la virusi vya Corona ilishindwa kuwasainisha katika dirisha lililopita kutokana na bei walizokuwa nazo lakini mwisho wa msimu huu wanaweza kufanikisha mchakato huo wa kuwasainisha.

Koeman alipoulizwa kuhusu jambo hilo alithibitisha kwa kusema “Uhitaji wetu kwa Wijnaldum ni mkubwa na wala sio tetesi, tunataka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa kuwa anauwezo mkubwa wa kucheza kati ya eneo la kiungo na safu ya ulinzi tena kwa kasi kubwa,”alisema.

“Niliongea naye na kumshwishi ajiunge nasi lakini tatizo lilikuwa kwa uongozi wangu ambao ulishindwa kulipa ada yake ya usajili.