Kocha wa Simba atua Singida

Saturday January 12 2019

 

Kocha wa zamani wa Simba, Dragan Popadic ametangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Singida United.
Popadic ambaye amechukua mikoba ya kuinoa Singida United kutoka kwa Hemed Morocco hakuja pekee atakuwa na msaidizi wake Dusan Momcilovic.
Momcilovic ambaye amekuja kama kocha msaidizi atafanya kazi ya kuwa kocha ya viungo.
Mkurugenzi wa Singida, United Festo Sanga alisema mara baada ya kumtambulisha Popadic wanatangaza rasmi kuachana na Morocco ambaye ametingwa na majukumu mengi ya kutafuta vipaji kwa wachezaji wa timu ya Taifa.
Sanga alisema wamefanya mabadiliko mengine kocha wao msaidizi Shedrack Nsajingwa atakwenda kuwa kocha mkuu wa timu za vijana.
Anasema katika kuhakikisha Singida inafanya vizuri msimu huu katika mashindano ya Sport Pesa, Kombe la Shirikisho (FA) na Ligi Kuu Bara ndio wameamua kuboresha benchi la ufundi
"Tumeingia mkataba wa miezi sita na makocha wet hawa ukiwa na malengo matatu kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara, FA na SportPesa zaidi ya msimu ya vile tulivyofanya msimu uliopita katika mashindano yote," alisema.
"Makocha hawa wamekuja nchini kwa mara ya pili kwani walishawahi kufundisha Simba na tunaamini katika uwezo wataifikisha timu katika malengo yake," alisema Sanga.
Popadic alisema anakuja tena kufundisha soka Tanzania analifahamu maana amefundisha nchi nyingi za Afrika kwahiyo anaimani atafanya like ambacho kipo katika malengo ya timu.
"Tanzania kuna vipaji vingi vya soka bado sijaiona timu lakini naimani kubwa kutakuwa na wachezaji ambao wanauwezo na tukafanya yale ambayo nahitaji," alisema.
"Tusahau yale yaliopita ambayo nimeyafanya hapa nchini nikiwa na Simba nimekuja kuanza kazi upya," alisema Popadic.

Advertisement