Kocha Velverde amtetea Suarez Barcelona ikiua 5-1

Thursday March 14 2019

 

Ushindi mnono wa Barcelona wa mabao 5-1 dhidi ya Lyon umewapeleka hatua ya robo fainali, mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliopigwa Uwanja wa Camp Nou jana Jumatano usiku.

 Lionel Messi aliweka wavuni mabao mawili yaliyotinga dakika za 18 na 78. Pia Philippe Coutinho aliipatia bao timu yake dakika ya 31,  wakati Gerard Pique aliifungia timu yake bao dakika ya 81, huku Ousmane Dembele akiweka wavuni msumari wa mwisho dakika ya 86.

Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde amesifu kikosi chake kwa ushindi huo mnono, huku akimkingia kifua Luis Suarez baada ya kutimiza siku 343 kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa na ukame wa mabao.

Alisema anatambua watu wataanza kufuatilia takwimu za mchezaji huyo  za mabao kutokana na kushindwa kuweka wavuni mipira.

 

Advertisement