Kocha Simba asifu kambi Afrika Kusini

Muktasari:

Aussems ambaye alikuwa na kikosi hicho Uturuki msimu uliopita amesema, anafurahia mazingira hayo kwa sababu kila kitu kinapatikana pia ni tulivu.

KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesifu mazingira ya kambi yao iliyopo nchini Afrika Kusini.
Aussems ambaye alikuwa na kikosi hicho Uturuki msimu uliopita amesema, anafurahia mazingira hayo kwa sababu kila kitu kinapatikana pia ni tulivu.
"Mazingira ya kambi hapa ni mazuri kwa sababu kila kitu ambacho tunakihitaji kinapatikana kwa wakati. Lakini, kuna utulivu jambo linalofanya wachezaji kuweka akili yao sehemu moja na kuifanya kazi yangu kuwa rahisi,"anasema.
Simba imeweka kambi nchini hapa kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara pamoja na michuano mingine ikiwemo ya kimataifa ambapo wao wataiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ikiwa hapa inategemea kukaa kwa muda wa wiki mbili na kucheza mechi nne za kirafiki kabla ya kuondoka.