Kocha Simba asema wapo fiti kuivaa Mtibwa

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroek, amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili Mtibwa Sugar, katika mchezo  unaofanyika leo Jumamosi kwenye  Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kocha hugo raia wa Ubelgiji mesema wachezaji wake wote wapo fiti na morali ya kutosha kuhakikisha wanaendeleza ushindi baada ya kupata pointi tatu katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ihefu FC.

Pamoja na kukiri Mtibwa Sugar ni timu ngumu, amesema kikosi chake kipo imara kukabiliana na wenyeji wao ili kuvuna pointi tatu, na  kuendelea kujitengenezea mazingira mazuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

"Najua mechi itakuwa ngumu kwasababu tunacheza ugenini, lakini nakiamini kikosi changu kitafanya kazi ya kuhakikisha tunaondoka na ushindi,"amesema Sven nakuongeza kuwa.

"Natamani kushinda mechi sita mfululizo, lengo ni kuandaa mazingira ya kuchukua ubingwa kwa mara nyingine, hivyo mchezo huu na Mtibwa Sugar,tumejipanga vya kutosha kuondoka na pointi tatu,"amesema.

Amesema silaha kubwa ya kushinda mechi na Mtibwa Sugar, all ni nidhamu na kujituma kwa bidii na kwamba hakuna njia ya mkato katika soka.

"Hakuna siri zaidi ya bidii na kuheshimu kazi, wachezaji wa Simba wanajua hilo, hivyo naamini tutatimiza malengo yetu ya pointi tatu,"amesema.