Kocha Simba amweka benchi Okwi

Muktasari:

Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amekifanyia mabadiliko kikosi chake kitakachoivaa Mwadui FC leo Jumapili na miongoni mwa wachezaji aliowapumzisha ni Emmanuel Okwi.

Shinyanga. Kocha Mkuu wa Simba,  Patrick Aussems amesema, kutomtumia mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi raia wa Uganda ni sehemu ya mipango yake ya ushindi.

Mechi iliyopita, Aussems alimwanzisha Okwi kwenye kikosi cha kwanza lakini mara kadhaa mashuti yake yaliyolenga golini hayakumpa matokeo mazuri wakafungwa na Mbao FC bao 1-0, mchezo uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Aussems amesema, ana wachezaji wazuri wengi anaowaamini na baada ya kuuangalia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga amegundua si rafiki kwao ndiyo maana akafanya mabadiliko hayo.

Katika kikosi chake kitakachoivaa Mwadui FC leo Jumapili ya Septemba 23, Mghana James Kotei ameanza kikosi cha kwanza wakati mechi iliyopita alikuwa benchi.

Mnyarwanda Meddie Kagere aliyeanzia benchi mechi ya Mbao FC ameanza huku Mohammed Ibrahim 'Mo Ibrahim' akianzia benchi.

 

KIKOSI CHA SIMBA

Aishi Manula

Mohammed Hussein

Shomary Kapombe

Erasto Nyoni

Paschal Wawa

Jonas Mkude

James Kotei

Cletus Chama

John Bocco

Meddie Kagere

Shiza Kichuya

 

WA AKIBA

Deogratius Munish 'Dida'

Paul Bukaba

Emmanuel Okwi

Adam Salamba

Mohamed Ibrahim

Rashid Juma