Kocha Simba akataa kampeni ya Do or Die

Friday March 15 2019

 

By CHARITY JAMES

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameikataa kampeni ya Do or Die aliyoianzisha afisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara na kuweka wazi kuwa kitu kama hicho hakipo katika mpira.

Aussems ametamka maneno hayo leo Ijumaa jijini Dar es Salaam na kuweka wazi kuwa wanawaheshimu wapinzani wao na wanaingia kwenye mchezo wakiwa na imani ya kutinga hatua inayofuata ya robo fainali.

"Tumeshinda michezo yote nyumbani tumecheza na JS Saoura tulipata matokeo tumecheza na Al Ahly tumeshinda na sasa ni AS Vita tutashinda pia,"alisema Aussems.
"Tunafahamu ni mchezo mgumu lakini tumejiandaa kwa ajili ya kushindana.
Nyota wangu wote wana hari ya mchezo wamejiandaa kwa ajili ya kushindana."


Amsema, wanatarajia kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ili waweze kuingia hatua ya robo fainali.

Advertisement