Kocha Polisi Tanzania awataka wachezaji kujitunza

Muktasari:

Waziri wa Tanzania, Kassim Majaliwa alitangaza kusitishwa na Ligi kuu Tanzania Bara ndani ya siku 30 kutokana na ugonjwa wa Corona.

Dar es Salaam.Kocha Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania Malale Hamsini, amewataka wachezaji wake kutumia vyema siku 30 watakazokuwa majumbani kwao.

Kocha Hamsini alisema ushauri wake kwa wachezaji wakazitumie vizuri hizo siku kwa kujifua wenyewe kila mtu kwa muda wake ili kujiweka fiti zaidi.

Alisema ni wakati wa wao kujitambua na kujua thamani yao sambamba na kuheshimu kazi yao, kwa kuwa mazoezi ya pamoja hayatakuwepo hivyo ni bora kila mchezaji ajitambue.

"Hili ni janga la kitaifa na ndio maana Serikali imezungumzia hivyo mimi kama kocha nilikuwa na plani zangu na hasa ikizingatia leo tungecheza, lakini ndio hivyo tena,"

Anasema kikosi chake kilikuwa katika hali ya juu kwa kila mchezaji hivyo siku 30 kutokuwa pamoja itaathiri ufundi, lakini hakuepukiki kutokana na tishio la gonjwa hilo.