Kocha Nkana: Sisi tuna Kessy wao Chama

Muktasari:

Mechi hiyo Simba na Nkana inakumbusha mechi ya Ligi ya Mabingwa 2002, katika mchezo wa kwanza uliofanyika mjini Kitwe Nkana ilishinda 4-0, lakini katika mechi ya marudiano iliyofanyika Morogoro, Simba ilishinda 3-0, lakini Nkana ilisonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.

Dar es Salaam. Kocha wa Nkana Beston Chambeshi amesema Simba wana Clatous Chama na sisi tuna Hassan Kessy hivyo mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa utakuwa mgumu.

Miamba hiyo ya Kitwe imefanikiwa kusonga mbele kwa mashindano hayo baada ya kuifunga UD Songo kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya mchezo wa nyumbani kushinda 1-0, wakati ule wa ugenini wakishinda 2-1.

Nkana sasa itacheza na Simba katika mechi ya kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa itakayochezwa kati ya Desemba 14 na 16 nchini Zambia.

Kocha huyo alipoulizwa kuhusu mechi yake ijayo dhid ya Simba Simba, Chambeshi alisema mechi hiyo naiona ipo 50/50.

Aliongeza kuwa kwa sasa mashabiki wa Nkana wanazungumzia kuhusu Simba ndivyo ilivyokuwa kwa Nkana inavyozungumziwa Tanzania.

“Naitazama Simba. Nafikiri wanazungumza kuhusu Nkana. Kwa hiyo mechi hii ni 50/50. Wanamchezaji kutoka Zambia na sisi tunamchezaji kutoka Tanzania. Tunachokihitaji kwa sasa ni kujiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo,” alisema Chambeshi.

Beki Hassan Kessy amekuwa katika kiwango kizuri tangu alipotua Zambia na kujiunga na miamba hiyo ya Kitwe mapema mwaka huu.

Kessy amecheza mechi zote mbili za Ligi ya Mabingwa dhidi ya UD Songo, huku akifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Barclays.

Wakati Kessy akitamba Zambia ndivyo ilivyokuwa kwa Chama tangu ametua Simba amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania.

Chama aliingoza Simba kuichakaza Mbabane Swallows akiwa amefunga mabao matatu na kutegeneza matatu katika ushindi wao wa jumla wa mabao 8-1.

Wakati huo huo, CAF imeweka wazi ratiba ya mechi zote za raundi ya kwanza za Ligi ya Mabingwa zitakazochezwa wiki wa Desemba 14 na 16, na marudiano yatakuwa siku saba baadaye.

Mechi za kwanza:

Nkana (Zambia) vs Simba (Tanzania)

Constantine (Algeria) vs Vipers (Uganda)

Orlando Pirates (RSA) vs African Stars (Namibia)

TP Mazembe (DRC) vs Zesco United (Zambia)

Ismaily (Misri) vs Coton Sport (Cameroun)

Wydad Casablanca (Morocco) vs Jaraaf (Senegal)

Al Ahly Benghazi (Libya) vs Mamelodi Sundowns (RSA)

Al Ahly (Misri) vs Jimma Kenema (Ethiopia)

Stade Malien (Mali) vs Asec Mimosas (Ivory Coast)

AS Vita (DR Congo) vs Bantu (Lesotho)

Club Africain (Tunisia) vs Al Hilal (Sudan)

Otoho d’Oyo (Congo) vs Platinum (Zimbabwe)

Al Nasr (Libya) vs Horoya (Guinea)

Saoura (Algeria) vs IR Tanger (Morocco)

Gor Mahia (Kenya) vs Lobi Stars (Nigeria).

Mabingwa watetezi Esperance wa Tunisia wamefuzu moja kwa moja kwa hatua ya makundi wanachosubiri ni ratiba itakayopagwa mwisho wa mwaka huu.