Kocha Nigeria: Serengeti Boy imetupa mzuka kufuzu Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Nigeria imekuwa timu ya kwanza kufuzu kombe la dunia ambalo litafanyika Brazil baada ya kushinda mechi zake mbili katika michuano ya Afcon.

Dar es Salaam.Kocha wa Nigeria, Manu Garba amesema matokeo na walivyocheza katika mechi ya kwanza dhidi ya Serengeti Boys ndio yamewapa mzuka na kuwasukuma wachezaji wake kushinda mechi ya pili.

Katika mchezo wa pili, Nigeria imeifunga Angola kwa bao 1-0, na kufuzu kwa Kombe la Dunia Brazil.

Garba alisema mchezo wa kwanza dhidi ya Serengeti Boys walitengeneza nafasi nyingi za kufunga ambazo kati ya hizo walizitumia kufunga mabao.

Alisema tulifanya makosa na tukaruhusu kufungwa mabao manne ambayo tuliyafanyia kazi kabla ya mchezo wa leo.

"Baada ya kufanyia kazi ubora na mapungufu ambayo yalitokea katika mechi ya kwanza na Serengeti ndio yametupa morali ya ushindi katika mechi hii.

"Kimsingi tunafuraha kubwa kufuzu kombe la dunia na ushindi huu si wa wachezaji na benchi la ufundi bali Wanigeria wote," alisema Garba.