Kocha Milambo: Bado Serengeti Boys tuna nafasi

Muktasari:

  • Alisema kilichopo mbele yao ni kushinda mechi ya mwisho dhidi ya Angola na kama Nigeria ataishinda Uganda kuna hesabu zitafanyika.

Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo licha ya kupoteza mchezo wa pili dhidi ya Uganda amesema bado kuna nafasi ya kufuzu.

Mirambo alisema kupoteza mchezo huo kila Mtanzania imemuama kama ilivyo yeye na wachezaji wake.

Alisema kilichopo mbele yao ni kushinda mechi ya mwisho dhidi ya Angola na kama Nigeria ataishinda Uganda kuna hesabu zitafanyika.

"Matokeo kama yakienda hivyo nasi tukashinda mchezo wa mwisho ina maana tutabaki na pointi tatu, kama Uganda na Angola huku Nigeria akiwa amefuza na pointi tisa," alisema.

"Kwa maana hiyo sisi wenye pointi tatu kila mmoja kuna hesabu itafanyika na kuona kama tumeondolewa au bado.

"Kuhusu kama nimeshindwa kuipeleka timu katika fainali za Kombe la Dunia niachie nafasi hii sizani kama litakuwa jambo sahihi kwa maana nitakuwa nakimbia changamoto," alisema Mirambo.

 Serengeti walifungwa mechi ya kwanza na Nigeria kwa mabao 5-4, dhidi ya Nigeria na Uganda wakakubali tena kichapo cha mabao 3-0.

Kwa maana hiyo Serengeti katika mechi mbili walikubali kupoteza zote kwa kufungwa mabao nane na wao kufunga manne.