Kocha Lyon mjanja sana aisee

Sunday September 16 2018

 

By OLIPA ASSA

SOCCOIA Lionel, Kocha Mkuu wa African Lyon, mjanja sana kwani amefichua amekuwa akitumia mifumo tofauti katika mechi zao za Ligi Kuu na kwa bahati imewabeba, japo anakiri ule wa 4-4-2 nyota wake hawajaunasa vyema.

Lyon iliyocheza mechi nne na kupata sare tatu na kupoteza moja, ikiwa na alama tatu kibindoni na kumfanya Kocha Lionel kusema sare yao na Coastal Union ilitokana na mfumo wa 4-4-2 aliutumia, japo bado vijana wake hawajaupatia.

“Katika mechi inayofuata nitaangalia vijana kama hawatakuwa na uchovu basi nitautumia mfumo huu huu, nikiona hawapo fiti nitawabadilishia ili mradi tupata matokeo mazuri baada ya kutoka sare tatu mfululizo.

Naye straika wa timu hiyo Victor Da Costa, aliyecheza mbele sambamba na Haruna Moshi ‘Boban’ alisema kinachomsumbua kwa sasa ni hali ya hewa ya joto kali kwa madai alikotoka ni baridi lile la barafu, jambo hilo alidai linamfanya ashindwe kuonyesha makali yake.

Advertisement