Kocha Kenya atangaza jeshi la kuivaa Taifa Stars

Muktasari:

Kikosi cha Harambee Stars ni mchezaji mmoja tu aliyekwenda Afcon Misri ametwaa kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanzania

Nairobi, Kenya. Kocha wa Kenya ‘Harambee Stars’ Sebastien Migne ametangaza kikosi cha kwanza cha wachezaji 24, kujiandaa na mechi mbili dhidi ya Tanzania za kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN2020).

Katika kikosi hicho beki Gor Mahia, Joash Onyango ni mchezaji pekee aliyeitwaa ambaye aliyekuwa katika kikosi cha Kenya kilichoshiriki fainali za Afcon 2019, Misri. AFCON finals in Egypt.

Kikosi hicho kimewachukua makipa wawili ambao ni kipa wa Kariobangi Sharks, John Oyemba na James Saruni wa Ulinzi Stars.

Mabeki katika kikosi ni; Philemon Otieno (Gor Mahia), Yusuf Mainge (AFC Leopards), Joash Onyango (Gor Mahia), Benard Ochieng (Wazito), Mike Kibwage (KCB), Andrew Juma (Mathare United) na David Owino (Mathare United).

Dennis Odhiambo (Sofapaka), Teddy Osok (Wazito), Kenneth Muguna (Gor Mahia), Duke Abuya (Kariobangi Sharks), Patillah Omoto (Kariobangi Sharks), Paul Were (AFC Leopards), Samuel Onyango (Gor Mahia), Roy Okal (Mathare United) na Whyvone Isuza (AFC Leopards) wanategeneza safu ya kiungo.

Washambuliaji; John Avire (Sofapaka), Musa Masika (Wazito), Nicholas Kipkirui (Gor Mahia), Sydney Lokale (Kariobangi Sharks), Piston Mutamba (Wazito) na Enosh Ochieng (Ulinzi Stars).

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mchezo wa kwanza utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Julai 26-28, 2019.

Mechi ya marudiano itachezwa siku chache baadaye jijini Nairobi.

Mshindi wa mchezo kati ya Tanzania na Kenya atacheza na mshindi wa mechi kati ya Burundi na Sudan Kusini kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika Cameroon kati ya Januari na Februari 2020.

Makipa: John Oyemba (Kariobangi Sharks), James Saruni (Ulinzi Stars)

Mabeki: Philemon Otieno (Gor Mahia), Yusuf Mainge (AFC Leopards), Joash Onyango (Gor Mahia), Benard Ochieng (Wazito), Mike Kibwage (KCB), Andrew Juma (Mathare United), David Owino (Mathare United)

Viungo: Dennis Odhiambo (Sofapaka), Teddy Osok (Wazito), Kenneth Muguna (Gor Mahia), Duke Abuya (Kariobangi Sharks), Patillah Omoto (Kariobangi Sharks), Paul Were (AFC Leopards), Samuel Onyango (Gor Mahia), Roy Okal (Mathare United), Whyvone Isuza (AFC Leopards)

Washambuliaji: John Avire (Sofapaka), Musa Masika (Wazito), Nicholas Kipkirui (Gor Mahia), Sydney Lokale (Kariobangi Sharks), Piston Mutamba (Wazito), Enosh Ochieng (Ulinzi Stars)

Ratiba ya ukanda wa Cecafa (raundi ya kwanza)

Burundi Vs Sudan Kusini – Bujumbura

Tanzania Vs Kenya – Dar es salaam

Djibouti Vs Ethiopia – Djibouti

Somalia Vs Uganda – Mogadishu

Marudiano Agosti 2, 2019

Raundi ya pili:

Mechi ya kwanza: Septemba 20-22

Mechi ya marudiano: Oktoba 18-20