Kocha Hispania amwaga chozi mbele ya wachezaji

Muktasari:

Kocha wa Hispania Roberto Moreno amelia mbele ya wachezaji wake baada ya kumalizika mchezo wa kimataifa baina yao na Romania.

Madrid, Hispania. Roberto Moreno ameshindwa kuzuia hisia zake kwa wachezaji wake baada ya kumwaga machozi katika mchezo dhidi ya Romania.

Licha ya kupata ushindi wa mabao 5-0 wa kufuzu fainali za Kombe la Ulaya, kocha huyo alitoa machozi alipokuwa akiaga wachezaji wake

Kocha wa zamani wa timu hiyo Luis Enrique aliyekuwa akihusishwa na mpango kutua Arsenal, anatajwa kurejea katika kikosi hicho.

Moreno, aliyerithi nafasi hiyo kwa Enrique ambaye alijizulu baada ya kufiwa na mwanaye, anadaiwa uwezo wake umefika ukingoni.

Mtoto wa nguli huyo wa zamani wa Hispania Zana alifariki kwa ugonjwa wa kansa akiwa na miaka tisa.

Chama cha Soka Hispania jana kilitarajia kutangaza kumuondoa Moreno na kumtangaza Enrique kocha mpya.

Moreno (42), aliyeshinda mechi saba kati ya tisa juzi hakuingia ndani ya ukumbi kuzungumza na vyombo vya habari licha ya kuipelea Hispania katika fainali hizo.

Hata hivyo, idadi kubwa ya wachezaji walishitushwa na taarifa za kocha huyo kuondoka, lakini walimtakia kila la kheri.