Kocha Emery aambiwa, sajili mtu fasta

Muktasari:

Mapema Arsenal ilimchukua Sven Mislintat lakini mshambuliaji huyo haina mpango wa kumsajili dirisha la Januari.

LONDON, ENGLAND.MABOSI wa Arsenal wamepiga hesabu, wakaona Danny Welbeck haponi leo wala kesho, wakamwambia kocha wa timu hiyo, Unai Emery, tafuta mtu.

Welbeck alianguka vibaya kwenye mchezo wa Michuano ya Europa League dhidi ya Sporting Lisbon na kuumia enka.

Bosi wa Arsenal ambaye pia ni Mkurugenzi wa Soka, Raúl Sanllehi alimwambia Emery kuwa atafute mtu wa kuziba nafasi yake kwa kuwa Welbeck kuumia kwake si kwa kupona leo wala kesho.

Mapema Arsenal ilimchukua Sven Mislintat lakini mshambuliaji huyo haina mpango wa kumsajili dirisha la Januari.

Hata hivyo, Sanllehi alisema kuwa hakuna namna kwani klabu inalazimika kusajili mbadala wa Welbeck kwa kuwa ameumia kwa kiasi kikubwa.

‘Hii haikuwa kwenye mipango, tutalazimika kufanya usajili ambao hatukuupanga,” Sanllehí aliliambia gazeti la Independent. ‘Tumneumizwa na Danny na tutampa sapoti zote. Hii inatufanya tufikirie zaidi.” ‘Sisemi kwamba ni wakati wa kujiachia, hii ni dharula, tunawachezaji wengi wazuri, lakini hii ya kusajili tumemwambia afanye kwa kuwa tunaweka akiba.

‘Hatutafunga milango, lakini kwa sasa tunaka kusajili mchezaji mmoja na wengine tunaowachagua tutafanya hivyo baadaye.”