VIDEO: Aussems afunguka ishu ya kuumia Erasto Nyoni

Muktasari:

Nyoni aliumia mguu baada ya beki wa KMKM, Hafidh Mohamed kumgonga goti.
Viongozi wa Simba walilazimika kumpeleka hospitali mchezaji wao kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems amethibitisha beki wa Erasto Nyoni  kuwa ni majeruhi na atarejea uwanjani Februari.
Nyoni aliumia mguu baada ya beki wa KMKM, Hafidh Mohamed kumgonga goti.
Viongozi wa Simba walilazimika kumpeleka hospitali mchezaji wao kwa ajili ya matibabu zaidi.
Mtoni aliumia dakika ya 41 baada ya kugongana, hivyo kocha Patrick Aussems kulamizika kumuingia kiungo Said Ndemla. 
Mchezo huo wa Simba juzi, uliisha kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-1. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara jana Jumatatu alikanusha kwenye mitando ya kijamii na kusema mchezaji huyo sio majeruhi.