Kocha Zanzibar aita 38 kujiandaa Chalenji

Muktasari:

 

  • Timu hiyo itaingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Chalenji kwa vijana chini ya miaka 20.

Zanzibar. Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, Salum Ali Haji, ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 38, kwa ajili ya kujiandaa na Mashindano ya Cecafa ya Vijana yanayotarajiwa kufanyika Uganda Desemba 15-25, 2018.

Kocha Salum ametangaza kikosi hicho kwenye Ukumbi wa uwanja wa Amaan Mjini Unguja katika mkutano.

Walioitwa kuunda kikosi hicho upande wa Makipa yupo, Peter Dotto Mashauri (Black Sailors), Abdulattif Said Masoud (Jamhuri), Mwinyi Ali Mwinyi (Mapembeani) na Yakoub Suleiman (Muembeladu).

Mabeki: Khalid Khamis (Simba FC ya Zanzibar), Abdul hamid Ramadhan (Villa Fc), Abdulhakim Khamis Faki (Sporting FC), Abubakar Suleiman (ZFDC), Mudathir Nassor (New Afrika), Salum Suleiman (Kimbunga Fc) Ahmada Khamis Amour (Kinyasini), Shaabani Pandu (Villa United), Omar Haji Chareli (Mlandege), Abdul salami Habibu Ubwa (Villa United) na Ame Ali Khamis (Villa United).

Viungo: Arif Mohd Said (Opec), Fahad Mussa Hassan (Mapembeani), Eliyass Suleiman (KMKM), Nassir Sheha Abdallah (Opec), Mohd Mussa (Malindi), Yahaya Silima (ZFDC), Abdul hakim Naimu (Villa United), Khalid Habib Iddi (Mpapa Star), Mohd Ramadhan Khamis (Villa United), Mohd Issa Simai (Happy kids), Bakar Ajuwed Jaffar (JKU Academy) na Rakib Mohd Ali (Freedom Kids).

Washambuliaji: Faki Abdallah (JKU Academy), Hussein Mohd Khamis, (New Afrika), Said Salum Khamis (Taifa ya Jangombe), Mohd Daud Suleiman (King Boys), Abdillah Haji Khamis (Opec), Ibrahim Ali "Chafu" (Mlandege), Omar Ame Omar (Kwerekwe City), Abdul hamid Juma "Samata" (Mlandege) na Ramadhan Makame (Yambone).