Kocha: Yondani alikuwa lazima akae benchi Mwantika acheze!

Muktasari:

Baada ya timu ya Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Cape Verde kuna baadhi ya wadau wa soka wamekuwa wakimtupia lawama Kocha Mkuu Emmanuel Amunike kwa nini alimweka Kelvin Yondani bechi na kumchezesha beki kama David Mwantika.

Dar es Salaam. Kenny Mwaisabula amewaambia wadau wa soka watulie na waache lawama ya kumsema Kocha wa Taifa Stars, Mnigeria Emmanuel Amunike kwa nini alimweka Kelvin Yondani 'Vidic' nje na kumcheza mtu kama David Mwantika  katika mchezo wao na Cape Verde uliopigwa nchini huo.
Mwaisabula ambaye ni kocha wa aliyepita kwenye timu nyinyi ikiwemo Yanga amesema, kilichofanyika ni masuala ya kiufundi hata kama walifungwa mabao 3-0.
"Kocha yeyote hawezi kubadilisha timu yake iliyofanya vizuri na kuingiza wachezaji wapya ndiyo maana uliona katika kikosi cha Taifa Stars kilichocheza na Uganda 'The Cranes' mtu pekee aliyeanza tofauti na wale ni Himid Mao tu baada ya Frank Domayo kuumia,"alisema Mwaisabula.
Ameongeza na kusema, hivyo, halikuwa jambo rahisi kumtoa Mwantika katika mchezo na Cape Verde kwa sababu alifanya vizuri mechi na Uganda mchezo ambao Yondani hakuwepo kwa sababu ya majeruhi.
Amekwenda mbali na kufafanua ili kuthibitisha anachokiongea ni kweli, timu itakayocheza na Cape Verde mechi ya marudiano itakuwa na mabadiliko makubwa kutokana na aina ya matokeo yaliyopatikana.
Katika mchezo wa Taifa Stars na Uganda uliopigwa nchini Uganda, ulimalizika kwa suluhu.