Klopp aitega Atalanta, Kaita, Matip wakirejea

LIVERPOOL, ENGLAND. KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp ameonyesha kuipa heshima yake Atalanta B.C. ambao watacheza nao leo Novemba 3 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kabla ya kikosi cha Liverpool kusafiri jana mchana na kwenda Italia, Klopp alizungumza na vyombo vya habari na kueleza mambo kadhaa kuhusiana na mchezo huo, ikiwemo urejeo wa baadhi ya nyota wake.

“Naby Keita na Joel Matip walifanya mazoezi jana, Thiago hakufanya hayo ndo mazingira yalivyo bado sijawa na maamuzi ya moja kwa moja juu ya kuwatumia ni jambo jema kufanya mazoezi kuliko kutofanya kabisa lakini ngoja tuone nini kitatokea," amesema na kuongeza.

"Huu mchezo ni mgumu kwa sababu tunakutana na timu bora kwenye kundi ni muhimu kwetu kuhakikisha tunapata pointi tatu ili kuwa na nafasi zaidi ya kusonga mbele," amesema.

Katika michezo yao iliyopita, Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wagonga nyundo wa London, West Ham United (Oktoba 31) huku katika mchezo huo kikosi chao kikiundwa na Alisson, Alexander-Arnold, Phillips, Gomez, Robertson, Henderson, Wijnaldum, Jones, Mane, Salah, Firmino.

Atalanta ambao walitoa dozi kwa Crotone ya mabao 2-1 wakiwa ugenini (Oktoba 31)na chama lao liliundwa na  Sportiello, Hateboer, Toloi, Romero, Djimsiti, Mojica, Freuler, Pasalic, Malinovskyi, Gomez, Muriel.