Klopp: Sijaiadhiri Bayern Munich, Liverpool imeshinda

Muktasari:

 

  • Alisisitiza kwamba hakutaka kuitandika Bayern Munich lakini alitaka Liverpool ishinde mchezo huo.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kwa mara nyingine tena timu yake imeonyesha maajabu kwa kutinga hatua ya robo fainali ikishinda ugenini mabao 3-1 Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Jumatano usiku.

Timu ya Liverpool imetinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuizamisha Bayern Munich mabao 3-1 kwenye  Uwanja wa Allianz Arena.

Mabao ya Liverpool yaliwekwa wavuni na Sadio Mane  dakika za (26 na 84), Virgil van Dijk  dakika ya (69)  huku bao pekee kwa Bayern Munich likifungwa na Joel Matip dakika ya (39).

Timu hiyo ya England imeendeleza ubabe kwa timu za Ujerumani ikiwa ni siku moja baada ya Schalke kufumuliwa mabao 7-0 dhidi ya Manchester City huku Tottenham nao walitangulia robo fainali baada ya kuiondoa Borrussia Dortmund.

Hivyo Liverpool imesonga mbele hataua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 3-1.

Klopp alisema hayo ni mafanikio makubwa kwa klabu yake kwa kuiondoa Bayen Munich kwenye mashindano hayo  barani Ulaya.

Alisema alitambua kwamba walikuwa na nafasi ya kushinda lakini hakuamini kile kilichotokea. Hata hivyo kikosi chake waliwezesha kile kilichotokea uwanjani.

Alisisiza kwamba hakutaka kuitandika Bayern Munich lakini alitaka Liverpool ishinde mchezo huo.